˸

Slaus Technologies Tz1 Admin Slaus Technologies Tz1 Admin Author
Title: RC Makonda afunguliwa Mashtaka Matano
Author: Slaus Technologies Tz1 Admin
Rating 5 of 5 Des:
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amemfungulia mashitaka matano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo ameyawasili...
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amemfungulia mashitaka matano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo ameyawasilisha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Makonda ni pamoja na kughushi vyeti, kupokea zawadi bila kutangaza, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma, kujipatia mali kutoka kwa watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, kuwadhalilisha watu kwa kuwataja kwenye tuhuma za madawa ya kulevya bila kuwa na vielelezo na kutumia madaraka vibaya.

Hatua hiyo ya meya Jacob, imekuja siku chache baada ya mkuu huyo wa mkoa, kudaiwa kuvamia kwenye ofisi za Clouds Media, kushinikiza kipindi kilichorekodiwa kikiwa na habari ya Mchungaji Josephat Gwajima, kirushwe hewani wakati kipindi cha Shilawadu kikiendelea.

Kitendo hicho kilimlazimu Waziri Nape Nnauye, mwenye dhamana ya kuwalinda waandishi wa habari, aunde tume maalum kuchunguza sakata hilo, ambayo ilipewa muda wa saa 24 kukamilisha kazi yake, lakini mpaka sasa bado ripoti yake haijatoka.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top